Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara, (CBE), Profesa Emmanuel Mjema akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la kitaaluma litakalofanyika Dodoma hivi karibuni. Kushoto ni Naibu Mkuu wa chuo Taaluma, Profesa Tandi Lwoga na kulia ni Naibu Mkuu wa chuo, anayeshughulikia Mipango na Fedha Dk. Emmanuel Munishi
Mkuu wa chuo hicho, Prof. Emmanuel Mjema amesema kuwa mahafali ya 57 ya cha ElChuo cha Elimu ya Biashara (CBE) yanatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mnamo Novemba 12 mwaka huu ambapo kutakuwa na wahitimu wa Shahada ya Uzamili, Stashahada ya Uzamili, Shahada ya Kwanza, Stashahada na Cheti cha Ufundi.
Pia amesme kuwa chuo hicho kimeandaa kongamano la maendeleo ya biashara na uchumi ambalo linatarajaiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi mkoani Dodoma.
Hayo yamesemwa chuoni hapo na Mkuu wa chuo hicho, Prof. Emmanuel Mjema, wakati akizungumzia kongamano hilo litakalofanyika tarehe 15 na 16 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani humo.
Alisema kongamano hilo linakauli mbiu ya ‘Biashara Uwekezaji na Ubunifu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi na kwamba kutokana na umuhimu wake viongozi mbalimbali wa Tanzania bara na visiwani watashiriki kongamano hilo.
Prof. Mjema alitaja mada zitakazojadiliwa kwenye kongamano hilo kuwa ni pamoja na Biashara ya ndani na kimataifa, Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni, Ubunifu na Ujasiriamali, Uwezeshaji wa Biashara na Ushirikiano wa Kiuchumi, uwekezaji na Teknolojia, Uchumi wa Buluu, Zuia mnyororo na Fedha za kidijitali
Alisema wiki ya Makongamano kwa Kampasi zote shughuli zitaanza Jumatatu hadi Alhamis ambayo itakuwa ni siku ya kilele na kwamba katika wiki hiyo shughuli mbalimbali kama vile mawasilisho ya machapisho, maonesho ya Idara za Kitaaluma ambayo yawahusisha wahitimu wa zamani yaani CBE Alumni ambao wanakaribishwa kuonesha bidhaa na huduma wanazozifanya.
“Pia semina na warsha kuhusu mambo mbalimbali ya biashara zitawezeshwa bila gharama yoyote na katika mahafali hayo ya 57 katika Kampasi zetu zote takribani Wahitimu 2,000 watatunukiwa stahiki zao katika ngazi tofauti tofauti,” alisema Profesa Mjema